
Ukiwapa watu kile wanachokitaka wataendelea kukihitaji.
Quoted by Enock Maregesi

Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo.
Quoted by Enock Maregesi

Mungu haamui jinsi watu wanavyoamua. Mtu akikwambia huna kipaji muulize yeye ni nani.
Quoted by Enock Maregesi

Usidharau midomo ya watu. Kuna watu wanaona mbele.
Quoted by Enock Maregesi

Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.
Quoted by Enock Maregesi

Watu wakiwa wamekasirika ongea nao jibu; usiongee nao tatizo.
Quoted by Enock Maregesi

Ubinadamu una kila kitu isipokuwa upendo miongoni mwa watu.
Quoted by Enock Maregesi

Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.
Quoted by Enock Maregesi

Usuluhishi ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu.
Quoted by Enock Maregesi